Mbio za Mwenge wa Uhuru leo zimefika Butiama. Kama desturi ya mbio za mwenge katika miaka tangu kufariki Mwalimu Nyerere mwaka 1999, ratiba ya mwenge kila mwaka inahusisha kupitisha mwenge kwenye makazi ya Mwalimu Nyerere yaliyopo Mwitongo, Butiama.
Kukaribisha mwenge leo Mwitongo alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, akiongoza baadhi ya wakazi wa kijiji cha Butiama.
|
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, (mwenye shati la kijani) akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Geoffrey Ngatuni, kwenye tukio la mwenge kupita Mwitongo, Butiama. |
|
Mwenge ukiingia Mwitongo, Butiama. |
|
Makongoro Nyerere akipokea mwenge toka kwa mkimbizaji mwenge, Flatei Massay |
|
Ulinzi wa mwenge siyo wa kawaida. |
|
Ulinzi wa mwenge siyo wa kawaida. |
|
Kiongozi wa mwenge, Dk. Nassoro Matuzya, akipandisha mwenge eneo la mwenge wa Mwitongo. |
Kabla ya risala iliyotolewa na kiongozi wa mbio za mwenge, Dk. Nassoro Matuzya, Mwenge wa Uhuru ulipandishwa kwenye eneo ulipo mwenge wa Mwitongo ili kuwasha mwenge wa Mwitongo kwa kutumia Mwenge wa Uhuru.
Wakimbizaji mwenge baadaye walizuru kaburi la Mwalimu Nyerere lililopo Mwitongo.
No comments:
Post a Comment