Tembelea Butiama

Tembelea Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Karibu Butiama / Welcome to Butiama

Kurasa Muhimu

Friday, September 3, 2010

Wageni toka JKT wamtembelea Mama Maria Nyerere

Leo asubuhi, wageni wanne toka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walimtembelea Mama Maria Nyerere kijijini Butiama.
Kutoka kushoto: Col. S.M. Msindo, mwenyeji wao na Mkuu wa Kambi ya JKT Rwamkoma, Lt.Col. Mlawa, Maj. M.M. Kipakulo, Maj. M.P. Kivuyo, na WO2 Daria Malombe.
Lt.Col. Mlawa, Mkuu wa Kambi ya JKT Rwamkoma akiwapa wageni maelezo nje ya kaburi la Mwalimu Julius K. Nyerere, Mwitongo, Butiama.
Baada ya kuzuru kaburi la Mwalimu Nyerere, wageni walitembelea Makumbusho ya Mwalimu J.K. Nyerere na kabla ya kuondoka walionana na Mama Maria Nyerere, mjane wa Mwalimu Nyerere.

Wageni pamoja na mwenyeji wao wakiwa pamoja na Mama Maria Nyerere, wa pili kutoka kushoto.



Wageni hao toka Dar es Salaam walikuwa kwenye ziara ya kikazi.

1 comment:

Anonymous said...

Utumishi wa Mwalimu kwa taifa letu ulikuwa adilifu. Ni wapi katika dunia hii watu bila kulazimishwa au kwenda kutalii wanalizuru kaburi la kiongozi wa nchi kama njia ya kumuenzi na kutoa heshima zao kwa kazi alizozifanya kwa taifa lao? Ni wapi katika dunia hii hotuba na maandiko ya kiongozi wa nchi yanaendelea kuliongoza taifa? Yale anayoyasema Mwalimu utadhani yu pamoja nanyi wakati huo katika maisha na changamoto zinazotukabili kama taifa-nchi. Hakika kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa babu huyu ambayo naamini yanaweza kuleta ukombozi wa pili na wa kweli kwa Afrika na mwafrika. Na huu ni ukombozi wa kiuchumi na kifikra inshallah.

Aruta Kontinua

Amani Millanga